Aureus wa Mainz

Mt. Aureus, Heilbad Heiligenstadt.

Aureus wa Mainz (alifariki 451 hivi) alikuwa askofu wa kwanza kujulikana wa Mainz, leo nchini Ujerumani, katika nusu ya kwanza ya karne ya 5, akitokea Ufaransa ya leo.

Alidhulumiwa kwa kutetea imani sahihi ya Kanisa Katoliki dhidi ya Waario na hatimaye aliuawa na wavamizi Wahunni Wapagani wakati wa kuadhimisha Misa[1].

Anaheshimiwa kama mtakatifu mfiadini pamoja na dada yake Yustina na wenzao.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 16 Juni[2].

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/57430
  2. Martyrologium Romanum

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by Tubidy